Kwa nini kuna makanisa mengi hivi?

Achilia mbali tofauti za makanisa na madhehebu maelfu elfu, yakitofautiana kiimani na matendo duniani leo, mara nyingi tunachanganyikiwa na kuachwa midomo wazi. Ni kanisa lipi liko “sahihi?” Ni kanisa lipi limeidhinishwa na Mungu? Ni kanisa lipi lilianzishwa na Kristo? Katika Matendo 2, tunasoma habari za kanisa moja lililoanzishwa na Yesu Kristo na kuidhinishwa na Mungu. Makundi mengi ya kidini yamejitenga toka katika kanisa la karne ya kwanza, yakimeguka na kuwa madhehebu mbalimbali tuyashuhudiayo leo. Ikiwa tunataka kuwa kanisa moja alilolianzisha Yesu Kristo karne ya kwanza, sawa na linavyotajwa katika Matendo 2, ni lazima tuweke pembeni miongozo, mafundisho na mapokeo ya binadamu, kisha kuwa kanisa moja sawa na lile tunalolisoma katika Agano Jipya.

 


 

For more information, please contact your local Church of Christ:

Scroll to top
Why Are There So Many Churches?